Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed ametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Masasi Oktoba 31, 2023.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Jida, Kata ya Jida, Halmashauri ya Mji Masasi unaotekelezwa kwa fedha za Sequip kwa gharama ya Tsh. 560,552,872, sambamba na Ukamilishaji wa Jengo la Dharula katika Hospitali ya Mkomaindo, Ukamilishaji wa Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Mkomaindo na Ujenzi wa Barabara ya Jida.
Aidha akihitimisha ziara yake, Mhe. Ahmed Abbas amewataka viongozi kwenda kusikiliza kero ya wananchi na kuzitatua, kusimamia ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya halmashauri sambamba na kutekeleza kwa wakati maagizo ya viongozi wakuu wa Serikali wanayoyatoa.
"Endeleeni kujenga utamaduni wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, narudia tena endeleeni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua". Mhe. Kanali Ahmed
Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake kwa kuzungumza na Viongozi ngazi ya Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Taasisi na wananchi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.