Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu ameongoza mkutano wa hadhara na wafanyabiashara wa soko la Mkuti Novemba 27, 2025.
Akizungumza katika mkutano huo, amehimiza kuhusu suala la usafi na udhibiti taka hususani kuhusu ulipaji wa gharama za uzoaji wa taka kwenye maeneo ya biashara iliyobadilika kutoka shilingi 200 hadi shilingi 300 kwa siku kwenye maeneo ya biashara kutoka Julai 2025 kutokana na gharama za huduma za uzoaji taka.

Aidha amewahimiza wafanyabiashara kulipa kodi ya pango la Halmashauri kwa wakati na mara baada ya kupokea changamoto kutoka kwa wafanyabiashara ya kukosa muda wa kufika Halmashauri, amewaahidi kusogeza huduma karibu kwa kufungua ofisi ndogo ya kutoa control number za malipo kwa wafanyabiashara katika soko la Mkuti.
Wakizungumza wafanyiabashara katika mkutano huo, wamesema suala la kufungua ofisi ndogo ya kulipia tozo mbalimbali katika soko hilo ni jambo kubwa, jema na lakupongezwa kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuendelea kupunguza madeni na kulipa kwa wakati.

MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.