Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Eliasi Ntiruhungwa Ambaye pia ni Mwenyekit wa Mtakuwa halmashauri ya Mji amewaomba wanajamii wa Masasi kupinga vitendo vya ukatili Kwa kutoa taarifa Idara husika pale yanapotokea Ili kutokomeza vitendo hivyo.
Ameyasema hayo September 23,2022 wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Mtakuwa ambayo yamehudhuriwa na wadau Mbalimbali wakiwemo wazee Maarufu , Viongozi wa dini ,Maafisa Elimu Msingi na Sekondari,Wafanyabiashara ,jeshi la Magereza,Jeshi la ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu wa Afya.
Mafunzo ambayo yamefadhiliwa na Shirika la @uniceftz na kuratibiwa na Mkurugenzi na afisa Ustawi wa jamii yenye Lengo la kukemea ukandamizaji wa Ulinzi na Usalama wa Mwanamke na Mtoto.
Katika Mafunzo hayo Mkurugenzi amewaomba wajumbe wote waliohudhuria kwenda kutoa Elimu Kwa jamii Kwa kutumia Makundi kuhusu ulizi na Usalama wa Mtoto na kukemea unyanyasaji ambao unaendelea katika jamii zetu.
Jamila Nassoro Mratibu Msaidiz wa Polisi ASP(Afisa dawati la jinsia) wilaya ya Masasi amewaasa wajumbe wa Mafunzo hayo kutoa Taarifa Mapema pale Changamoto inapotokea na kuonyesha Ushirikiano wa ushahidi pale panapohitajika kutolea Maelekezo Ili kutokomeza vitendo vya kikatili katika jamii.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.