Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni leo Februari 25, 2025 amezungumza na mamia ya wananchi na wafanyabiashara wa Wilaya ya Masasi katika Soko la Mkuti Halmashauri ya Mji Masasi ambapo ameeleza kuhusu mafanikio mbalimbali ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na miradi ya kimkakati inayotarajiwa kutekelezwa Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Mhe Kanoni amesema miongoni mwa miradi ya kimkakati ambayo inatarajiwa kutekelezwa ni Miradi ya TACTICS ambayo ina lengo la kuboresha miundombinu katika miji mbalimbali na inafadhiliwa na Benki ya dunia.
Amesema katika miradi hiyo Masasi imepata bahati ya kipekee ambapo kwa Halmashauri ya Mji Masasi ipo katika Kundi la tatu ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji ya Bunda TC, Handeni TC, Ifakara TC, Kasulu TC, Kondoa TC, Mafinga TC, Makambako TC, Masasi TC, Mbinga TC, Mbulu DC, Nanyamba TC, Newala TC, Nzega TC, Tarime TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Bagamovo DC, Chato DC.
Mhe Kanoni amesema kuwa Halmashauri ya Mji wa Masasi ikiwa kama wanufaika wa mradi huo wa TACTICS kupitia kundi la tatu imefanikiwa kupata miradi mitatu ambayo ni barabara zenye urefu wa kilometa 5.67 kwa kiwango cha lami ambazo ni adam viazi road, NMB anglican road, Makaburini road, Mtandi mission road, Napupa Mkuti road, Mpunga road na Masai Navai road ambazo zitachochea ukuaji wa Mji na kupendezesha Mji na kupunguza msongamano wa magari katikati ya Mji.
Amesema mradi mwingine ni ujenzi wa Stendi ya kisasa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 5.0412 lililopo eneo la Tokura kata ya Mwenge Mtapika ambao utasaidia kuongeza wigo wa biashara ya usafiri, Kuongeza wigo wa kibiashara kutoka mikoa Jirani, Mazingira rafiki na salama ya kufanyia Biashara na Kuimarika kwa ulinzi na usalama wa mali.
Amesema mradi wa tatu ni mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji wa Masasi katika eneo la Mkuti lenye ukubwa wa 4412m2 lilipo eneo la Mkuti kati kata ya Mkuti ambao una faida za kuongeza upatikanaji huduma kwa wanachi, Kufanya biashara katika mazingira rafiki na salama, Kutanua wigo wa kibiashara, Kuongeza mapato ya wafanyabiashara na Kuimarika kwa ulinzi na usalama wa mali.
Wakizungumza katika mkutano huo, Wananchi na wafanyabiashara wamesema wapo tayari kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa itakwenda kuinua Uchumi wa wananchi na Masasi yote kwa ujumla na kuongeza wigo wa ajira kwa wananchi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.