Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi Elias Ntiruhungwa November 14,2022 amefanya kikao na Madiwani ,watendaji wa kata ,Maafisa Elimu kata ,na Wakuu wa Shule wa Maeneo ambako Miradi inatekelezwa ya Sekta ya Elimu ,Afya chenye lengo la kutoa Maelekezo ya awali kuhusu mapokezi ya Fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mia sita arobaini na Nne laki saba na hamsini (644,750,000.00) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali katika kata zao.
Katika kikao hicho Ntiruhungwa alitoa Mchanganuo wa fedha hizo kwa kila Eneo la Mradi na Mradi ambao utatekelezwa kutokana na Fedha hizo na kuwaomba kila Afisa Mtendaji kata kwenda kufanya kikao na wananchi wake katika Maeneo yao kwa ajili ya kuwapa Taarifa ya Mapokezi ya Fedha hizo na Matumizi yake ili kuondoa changamoto mbalimbali ambazo huwa zinajitokeza kipindi cha utekelezaji wa Miradi.
Frenk Malanjila Diwani kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi kwa niaba ya Madiwani wote ametoa pongezi na Shukrani kwa Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuwaptia fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi kwa sekta ya Elimu,Afya na Utawala ameahidi kuwa wataenda kuzisimamia kuhakikisha Miradi inakamlika .
Kwa upande wake Kaimu Mkuu Idara ya ujenzi Ombeni Usiri amewaomba maafisa watendaji kata kwenda kusimamia Miradi hiyo kwa kila hatua ya Ujenzi kuanzia Michoro hadi hatua ya mwisho ili tuweze kufanikiwa kwa asilimia mia moja ya Utekelezaji .Aidha Mkurugenzi ametoa agizo kwa wasimamizi hao kwenda kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi wakati wa utekelezaji wa Miradi yao ili kurahisha kukamilika kwa haraka kwani anawaamini ni Viongozi wenye uweledi katika kusimamia Miradi na hawajawahi kumuangusha.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.