Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga Novemba 22, 2023 ameongoza zoezi la kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Mtwara vilivyotolewa na kampuni ya sigara ya TCC ikiwemo fimbo nyeupe, viti mwendo, cherehani za umeme na kawaida, mashine za kudalizi, baiskeli na magongo ya kisasa ya kutembelea kwa lengo la kuwasaidia kukidhi mahitaji yao.
Ametoa wito kwa wadau kuendelea kuunga mkono watu wenye mahitaji maalumu nchini ikiwemo kuwapatia vifaa saidizi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe, Kanali Ahmed Abbas amesema kuwa halmashauri zote tisa zimeguswa na baadhi ya taasisi za serikali ikiwemo shule na vyuo.
Meneja wa TCC mkoa wa Mtwara, Fredriki Masawe amesema wataendelea kuwafikia watu wote wenye mahitaji maalumu mkoani Mtwara.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.