Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Mji Masasi yamefanyika kwa kuhusisha wanawake kutenda matendo ya huruma kwa kutembelea Shule ya msingi kwa elimu jumuishi Masasi ambapo wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo magodoro na michango mbalimbali yenye jumla ya Tsh 600,000.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji, wakati wa kukabidhi michango hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Ndg. Rashid Njozi amesema ni muhimu jamii kukumbuka kutenda matendo ya huruma kwa watu wenye mahitaji maalumu kwakuwa wana mahitaji muhimu wanayoyahitaji kwa matumizi ya kila siku.
Amesema wanawake wameona ni vyema maadhimisho ya mwaka huu wajitoe kutenda matendo ya huruma kwa watoto wenye mahitaji katika shule hiyo na kuwa ni muhimu kila mwanajamii kutumia nafasi mbalimbali zilizopo kujitoa kwa chochote ulichonacho.
Maadhimisho ya mwaka 2024 yameongozwa na kauli mbiu ya "Wekeza kwa wanawake, kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".
Kauli mbiu "Wekeza kwa wanawake, kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".(Wawakilishi kutoka Halmashauri ya Mji Masasi katika picha ya pamoja wakati wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu March 08, 2024, Shule ya Msingi Jumuishi ya Masasi).

MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.