Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru Desemba 9,2022 Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imepanda miti zaidi ya 800 katika chanzo cha maji Mto Mbwinji kilichopo kijiji cha Nangoo Wilayani humo
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti Mkuu wa Wilaya ya Masasi Claudia Kita amesema wamejipanga kufanya shughuli mbalimbali za kiserikali ndani ya jamii na hii leo wameanza na kupanda miti katika chanzo cha maji lakini wataendelea na shughuli nyingine mbalimbali katika juma lote kuelekea tar 09 Desemba.
Aidha DC Kita ametoa agizo kwa mamlaka zinazosimamia chanzo hicho kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika wanafanya shughuli za kibindamu katita chanzo hicho kwani maji yanayozalishwa hapo ni msaada mkubwa na tegemeo kwa wananchi wa Wilaya za Masasi,Nachingwea na Ruangwa.
Kwa Upande wake Afisa ugani na uenezi wa TFS kanda ya kusini Andason Christian amesema wamekuwa wakishirikiana na wataalam wa mabonde ya maji katika kulinda misitu iliyopo katika vyanzo vya maji pamoja na kuhakikisha rasilimali zote za maji zinalindwa hivyo hatua ya upandaji miti katika mto huo utaendelea kuimarisha utunzaji.
Hata hivyo kwa upande wao mamlaka ya maji Masasi na Nachingwea Manawasa wamesema uamuzi uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi kupanda miti itasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa maji kwani kwa sasa chanzo hicho kinazalisha lita milioni kumi laki moja eflu nane mia nane na wakati wa masika huzalisha lita milioni 13.
Sanjari na hayo wananchi wanaozunguka chanzo hicho wameahidi kukilinda na kupeana elimu wao kwa wao .
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.