Ili viwanda viweze kuendelea katika uzalishaji wa bidhaa mbalilimbali na kuifanya nchi kufikia uchumi wa kati, vijana lazima wapewe elimu zaidi ya namna ya kutumia fursa ya kuwekeza katika kilimo. Mifugo na Uvuvi ili kuwezesha uzalishaji mkubwa wa malighafi ambazo zitatumika katika viwanda hivyo huku wao wakijiongezea uchumi
Msisitizo huo ulitolewa juzi na mgeni rasmi mhe Shaib Ndemanga rasmi wakati wa kufungua maonesho ya Nanenane kanda ya kusinikwa mwaka 2018 yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya lindi na kueleza kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo ni vema wakaelimishwa na kuwezeshwa kutambua fursa hiyo adhimu ya kuwekeza katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kama fursa ya kukuza uchumi wa nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe Selemani Mzee akisalimia Wananchi Waliohudhuria Sherehe za Ufunguzi wa Nanenane katika Viwanja Vya Nanenane Manispaa ya Lindi.
Mheshimiwa Ndemanga ameeleza kuwa maonesho ya nanenane kwa mwaka 2018 yameendelea kuonesha teknologia mbalimbali za kilimo mifugo na uvuvi, hivyo ni fursa nzuri kwa wananchi wote wa kanda ya kusini kwenda kujifunza njia za kisasa za uzalishaji wa mazao ya kilimo mifugo na uvuvi na hatimaye kuongeza uchumi katika jamii na taifa kwa ujumla.
“Tuanaamini, kama watu watalima, watafuga na kuvua kibiashara watazalisha ajira nyingi kwa wananchi wakiwemo vijana na hivyo kupunguza tatizo kubwa la ajira lililopo sasa, tumieni maonesho haya kama shamba darasa kujifunza teknologia mbalimbali ili muweze kuzalisha kwa tija” alisema Ndemanga
Ndemanga alifafanua kuwa zaidi ya 70% ya watanzania wanategemea sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi hivyo ni lazima sekta hizi ziboreshwe ili watanzania waweze kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ambalo ndilo lengo la serikali.
Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane 2018 inasema “wekeza katika kilimo,mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda” hivyo ni wajibu wa kila mtu kutambua fursa kwa kuwekeza ili kuzalisha malighafi za kutosha kwa ajili ya kuendeleza viwanda vya ndani na hatimaye kuisaidia serikali kupunguza gharama za kuagiza vitu kutoka nje ya nchi.
Aidha serikali imeendelea kufuta na kupunguza ada na tozo ikiwemo tozo 80 kati ya 139 za kilimo zimefutwa, kwenye ushirika tozo 20 zimefutwa na katika sekta ya mifugo tozo 7 zimefutwa ambazo zilikuwa kero kwa wakulima, wafugaji na wavuvi lengo ikiwa ni kuwapunguzia wakulima tozo na ada zisizo za lazima.
Moja ya Vitalu vilivyopo kwenye Banda la Halmashauri ya Mji masasi
Maonesho ya Nanenane kwa kanda ya kusini inashirikisha halmashauri 15 za mikoa ya lindi na Mtwara pamoja na taasisi zingine za serikali na binafsi, maonesho haya kwa kanda ya kusini yalianza rasmi kufanyika mwaka 2004.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.