Mradi wa Kituo cha afya Mtandi umehusisha ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwemo jengo la Opd, maabara, tanuru la kuchomea taka , jengo la upasuaji, jengo la kujifungulia na jengo la kufulia ambapo jumla ya Tsh milioni 500 zilitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.
Kituo cha afya Mtandi kilianza rasmi kutoa huduma tarehe 10/1/2023 mara baada ya kusajiliwa kikiwa na madaktari, wauguzi na manesi.
Ujenzi wa kituo cha afya Mtandi umetekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilianza baada ya kupokea jumla ya Tsh 250,000,000 ambazo zilijenga maabara, OPD, na ujenzi wa tanuru la kuchomea taka na awamu ya pili Halmashauri ilipokea Tsh milioni 250, 000,000/= kwa ajili ya jengo la upasuaji, jengo la kujifungulia na jengo la kufulia.
Kituo hicho kina vifaa tiba vya kisasa na bora, Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya Tsh milioni 350 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ambavyo vinatumika na bado vinaendelea kuletwa katika kituo hicho.
Ujenzi wa kituo cha afya Mtandi umepunguza adha ya wananchi kwenda umbali mrefu kupata huduma za afya. Takribani wananchi zaidi ya 30,000 kutoka ndani ya kata ya Mtandi na maeneo jirani ya kata za Mkuti, Jida, Napupa, Marika na Chanika nguo wanapata huduma katika kituo hiki.
Utoaji wa huduma za afya katika kituo cha afya Mtandi, ubora na vifaa tiba vya kisasa vimeendelea kuwashangaza wengi ikiwemo Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilipofika katika kituo hicho lakini pia Julai 15, 2024 Baraza la Wazee Masasi katika ziara yao Mbunge limeendelea kushangazwa na ubora wa kituo hicho huku likimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Ujenzi wa Kituo hicho cha kisasa na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini kwa jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma sambamba Baraza la Madiwani kwa kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unakuwa na Manufaa kwa wananchi.
Wakizungumza Katika ziara hiyo, wamesema mabadiliko waliyoyashuhudia ni yakistoria na kuwaomba wananchi wafike katika kituo cha Afya Mtandi kujionea wenyewe maboresho hayo makubwa ambayo hajayawahi kutokea kwa miaka mingi.
“Kwakweli katika ziara hii, tumefarijika sana kwa juhudi zake na usimamizi wake, Wito wangu wananchi wengine waje katika kituo hiki, ebu waje waonei ilivyobora, ilivyokuwa na mambo ya kisasa na yakuridhisha na sisi Masasi tusiite masasi, napenda tuiite (New Masasi) kwa maana ya Masasi, niwaombe wananchi wasiishie kusikia tu, waje wajionee wenyewe), Wamesema.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe Mwambe amesema mageuzi mbalimbali yamefanyika kuanzia majengo na vifaa tiba ili wananchi wa Masasi waweze kunufaika na huduma hizo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi, Mhe. Hashim Namtumba amesema kazi kubwa imefanyika katika maboresho hayo kilichobaki ni kubadili fikra na mitazamo kwa wananchi ambao bado wanamitazamo hasi za huduma za miaka ya zamani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu anatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi na kuleta watumishi wa afya katika halmashauri ya Mji.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.