Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi, Mwajabu Mkindi amewahimiza Waratibu Elimu
Kata na Waganga wa Vituo vya Afya kusikiliza kwa makini Mafunzo yanayotolewa ili wawe Walimu
Wazuri kwa Watumishi ambao wataenda kuwafundisha mara baada ya kumaliza Mafunzo haya.
Mgeni Rasmi aliyasema hayo Wakatio wa Ufunguzi wa Mafunzo ya UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA KWA
NGAZI YA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA Mafunzo ambayo yametafanyika kwa siku mbili katika ukumbi
wa Migongo Misheni.
Mgeni rasmi alisisitiza kuwa kuundwa kwa Mfumo Huu kutasidia kuhakikisha fedha za ruzuku
zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi, tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Vilevile ni kweli kuwa kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za raslimali fedha
zilizopo katika vituo vyetu vya kutoa huduma, na hivyo Halmashauri kushindwa kutoa taarifa sahihi za
matumizi ya ruzuku zinazotolewa katika vituo hivyo na wakati mwingine husababisha Halmashauri
husika kupata hati ya mashaka kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG).
Mfumo huu mpya sasa utasaidia kuhakikisha kunakuwa na muundo maalum wa kuhifadhi Taarifa za
Mapato na Matumizi, na hivyo kuongeza Uwazi na Uwajibikaji wa vituo vya kutolea huduma na hivyo
kupunguza changamoto mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza.
Pia mgeni rasmi alikumbusha matumizi ya Tovuti za Halmashauri katiak kuweka taarifa zote za Mapato
na Matumizi ya Fedha za umma. Suala Hili ni maelekezo ya Serikali, na kila mmoja wetu anapaswa
kutekeleza.
Mwisho mgeni rasmi aliwashukuru watu wa marekani kupitia Shirika la maendeleo ya Kimataifa la
Marekani ( USAID), pamoja na Mradi wa PS3, na Wadau wote waliohakikisha Mfumo huu unakuwepo,
ambao ni :Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha na
Mipango;Wizara Elimu,Sayansi,Technolojia na Ufundi , na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.