Kamati ya Ushauri ya wilaya (DCC) Agosti 24,2023 imekutana kwa ajili ya kikao maalum cha kupitia taarifa za Utekelezaji kwa kipindi cha Januari hadi Juni.
Akiongoza kikao hicho Mwenyekiti wa DCC ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Masasi Mh. Lauter John Kanoni amewaomba wajumbe kuishauri serikali mambo ambayo yataleta tija kwa maendeleo ya Halmashauri ya Mji Masasi.
Aidha Kanoni ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Mji Masasi kwa kuanzisha mchakato wa ukusanyaji na uzoaji taka kwa kumtumia Mzabuni na kuwataka wazabuni kuchapa kazi ili Mji wa Masasi uwe Msaafi na wenye Mazingira Mazuri.
"Hongereni saana Halmashauri ya Mji kwa kuanzisha mchakato huu kwani natumaini Mji wetu utakuwa msafi na wenye kuvutia lakini niwaombe na wazabuni wetu wachape kazi ili Mji uwe msafifi zaidi"Kanoni
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.