• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI HALMASHAURI YA MJI MASASI (DCC)

Posted on: January 20th, 2023


Kamati ya Ushauri Halmashauri ya Mji Masasi (DCC) January 20,2023 Imekutana katika kikao maalum cha kushauri Rasmu ya Bajeti ya Halmashauri ya Mji Masasi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akiongoza kikao hicho Mwenyekiti wa DCC ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mariam  Chaurembo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Masasi, amewaomba wajumbe kuishauri serikali kwa busara, “ushauri wenu ni tija kwa Maendeleo ya wilaya yetu” amesisitiza Mariamu Chaurembo.

Naye afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Masasi Wilfred Lazaro amesema kuwa Rasimu hii ya Bajeti imezingatia Dira ya maendeleo ya Taifa kufikia 2025, Mpango wa tatu  wa maendeleo  wa Taifa wa  miaka mitano (2021/2022-2025-2026).

Pamoja na Mambo mengine Bajeti hiyo imejikita katika kuleta matokeo chanya na yenye kugusa maisha ya Wananchi mmoja mmoja, Pia Bajeti, imejikita katika Miradi inayolenga kuzingatia malengo endelevu  ya mwaka 2030, aidha Lazaro ameieleza kamati kuwa Halmashauri inatarajia kutumia Shilingi  24,014,358,000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kati ya hizo Mapato ya ndani ni Shilingi  2,855,980,500  Ruzuku ya Matumizi ya kawaida na mishahara ni Shilingi 13,708,650,000  na  Miradi ya Maendeleo ni Shilingi 7,450,978,000.

Chaurembo amepongeza rasimu ya bajeti kwakuweka vipaumbele vya huduma za kijamii ambazo ni Elimu,Afya,na zinginezo ,pia  ameomba utekelezaji wa vipaumbele ufanyiwe kazi kwani kuwa na afya bora ndio mafanikio ya wanamasasi wote.

Wajumbe wa kamati ya ushauri nao wamepata muda mzuri na kushauri maeneo mbalimbali katika Rasmu ya Bajeti, Hivyo kikao kimekuwa na mafanikio makubwa zaidi kwani Bajeti inaaksi pia fursa kwa vijana na Wanawake, Rasimu hiyo ushauri wa DCC Utafikishwa kwenye kamati za kudumu za Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Masasi.

Kikao kimehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vya siasa, Viongozi wa Sekta binafsi, Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata zote, Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ,Wazee Maarufu,Viongozi,  Kaimu Mkurugenzi Jumanne Chaula  ambaye ni katibu wa kikao hicho na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu (DC) ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao hichi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA VITENDO VYA UKATILI DC MASASI

    March 08, 2023
  • ZINGATIENI MATUMIZI YA POS

    January 21, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI LIMEPITISHA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 24 HALMASHAURI YA MJI MASASI.

    January 21, 2023
  • KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI HALMASHAURI YA MJI MASASI (DCC)

    January 20, 2023
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.