Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amezindua rasmi kampeni ya upimaji wa maambukizi ya UKIMWI kwa wananchi waishio Mkoani Mtwara.
Kampeni hiyo ambayo inasimamiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ina lengo la kuhamasisha wananchi waishio Manispaa ya Mtwara-Mikindani pamoja na wale waishio Halmashauri ya Mji wa Masasi hususani wanaume kujitokeza kwenye upimaji wa virusi vya UKIMWI na kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi kwa wale wote watakaokutwa na maambukizi.
Pamoja na upimaji wa virusi vya UKIMWI kutakuwana upimaji wa magonjwa mengine kama Malaria, shinikizo la damu, sukari namagonjwa mengine.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo inayoenda na kaulimbiu isemayo "FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI" Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Mmanda ametoa wito kwa wananchi wote kujitokezakwa wingi kwenye upimaji ili kutambua afya zao na kuchukua hatua. Kampeni hii inategemea kufanya uzinduzi kama huo katika wilaya ya Masasi katika kata za mkuti tarehe 09/09/2018 mpaka 14/09/2018, na napupa 17/09/2018 mpaka 21/09/2018.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.