Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Said Nyengedi leo Januari 7, 2025 imetembelea miradi ya maendeleo iliyopo Halmashauri ya Mji Masasi na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Ndg. Nyengedi ameipongeza Halmashauri ya Mji Masasi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa huku akiwataka wananchi kutunza miradi hiyo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala ametoa pongezi zake za dhati kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kuzitaka Halmashauri zingine kuiga mfano mzuri uliooneshwa na Halmashauri ya Mji Masasi ili kuleta chachu ya maendeleo.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Matawale yenye thamani ya Tsh milioni 560 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP, Ujenzi wa Maegesho ya Magari Makubwa Mwengemtapika wenye thamani ya zaidi ya milioni 100 kutoka mapato ya ndani , Ujenzi wa Vyumba vitatu vya Madarasa na Matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi Mkuti B wenye thamani ya Tsh milioni 83,200,000 kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa BOOST na Ukamilishaji wa Ujenzi wa Bweni shule ya wanafunzi wenye mahitaji Maalumu Masasi, Milioni 50 kutoka mapato ya ndani
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.