Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dennis Londo imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Mtwara.
Kamati hiyo imeanza ziara yake kwa kupokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa ya miradi ya ujenzi wa miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kutembelea kituo cha afya cha Mtandi halmashauri ya Mji Masasi Novemba 13, 2023.
Kamati hiyo imepokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Bahati Geuzye katika ukumbi wa Jengo la utawala Halmashauri ya Mji Masasi.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Bi. Bahati amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kimkakati kama kiwanja kikubwa cha ndege cha kisasa kilichokarabatiwa kwa fedha kiasi cha Tsh bilioni 56, bandari ya Mtwara iliyopanuliwa kwa kujengewa gati jipya na kuwekwa vifaa vya kisasa, ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 210, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini na miradi mbambali ya vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha kamati hiyo imekagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD, Maabara na kichomea taka katika kituo cha afya Mtandi Halmashauri ya Mji Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.