Mkuu wa wilaya ya Masasi Mhe. Lauter John Kanoni amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) utakaofanyika Julai 13, 2023 katika viwanja vya sabasaba vinavyopatikana halmashauri ya mji Masasi.
Mhe Kanoni ametoa wito huo Julai 8, 2023 wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Tandale kata ya Jida, wafanyabiashara wa soko la Mti mwiba, na wafanyabiashara wa uwanja wa fisi kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wafanyabiashara.
Mhe. Kanoni amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili waweze kukuza biashara zao na serikali iweze kukusanya mapato.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Bi Erica Yegella amewataka wananchi na wafanyabiashara kuendelea kuzingatia usafi katika maeneo yao sambamba na kutoa fedha ya usafi ili kuboresha usafi na mazingira ya halmashauri ya Mji Masasi.
Mkuu wa wilaya katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero aliongoza na Mkurugenzi halmashauri ya Mji Masasi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Meneja TRA, Manawasa, Tanesco, Tarura.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.