Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Eliasi Ntiruhungwa amewaomba kamati ya afya ya Msingi ya Wilaya (PHC) ya chanjo ya Polio itakayoanza septemba 1,2022 Hadi September 4,2022 kuhakikisha zoezi hili la chanjo ya awamu ya tatu linaenda vizuri Ili kufikia malengo.
Ameyasema hayo Agost 31,2022 katika Kikao Cha Kamati ya Afya ya Msingi wilaya ya Masasi ya chanjo ya polio awamu ya tatu kilichowakutanisha wadau mbalimbali wilayani Masasi wakiwemo Viongozi wa dini ,wazee Maarufu pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.
Ameeleza kuwa Lengo la chanjo ya polio awamu ya tatu halmashauri ya Mji Masasi ni kuchanja watoto 17903 waliochini ya miaka mitano (5).
Sambamba na hayo ameitaka jamii ya Masasi kuongeza Kasi ya Usafi na kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo Bora Ili kuepuka Magonjwa mbalimbali hasa ugonjwa wa Polio.
Pia ametoa agizo kwa Viongozi wa Dini wote kwenda kutoa hamasa kwa jamii zinazowazunguka ili wazazi waweze kujitokeza katika zoezi hilo .
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.