Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Lauter John Kanoni ametoa agizo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri ya Mji Masasi kwenda kufanya Ufuatiliaji kwa watoto ambao wanahitimu Elimu ya Msingi ili kujua mienendo ya watoto hao.
Agizo hilo limetolewa Agosti 24,2023 katika kikao cha kamati ya Ushauri cha wilaya (Dcc) kilichofanyika ukumbi wa Mikutano uliopo Halmashauri ya Mji Masasi.
Aidha Kanoni ametoa Msisitizo kwa Maafisa Elimu kupitia shule zenye watoto wanaofanya vizuri katika Masomo yao na kufahamu maendeleo kama yako vizuri au yanamabadiliko ili yaweze kufanyiwa mikakati."Piteni shule zote zilizopo ndani ya halmashauri hii kuangalia maendeleo ya watoto wetu ili tujuwe kama wanafanya vizuri au kuna mabadiliko"Kanoni
Pia amewataka waalimu na viongozi kushirikiana katika ufuatiliaji huo kwani utasaidia kufahamu kama kuna usawishi wowote kutoka kwa wazazi ambao unasababisha watoto kufanya vibaya mitihani yao au vinginevyo.
"Kuna baadhi ya wazazi wanatabia ya kuwasawishi watoto wao wasifanye vizuri mitihani yao ili wafeli wasiendelee na Masomo yao hivyo niwaombe kila kiongozi akafanye ufatiliaji katika Eneo lake hii itasaidia kutambua changamoto zinazowafanya watoto kufeli katika Mitihani yao"Kanoni.
Kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (Dcc) kimehudhuriwa na wakuu wa Idara na Vitengo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ,watendaji kata ,Wadau mbalimbali ,wazee maarufu pamoja na Viongozi wz Dini.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.