Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas Ahmed amewaagiza wataalamu wa Halmashauri ya Mji Masasi kuhakikisha wanafanya tathimini ya kina ya vyanzo vya Mapato na kuitumia taarifa watakayoipata kubuni vyanzo vipya hatua ambayo amesema itasaidia kuijengea Halmashauri uwezo wa kutekeleza miradi yake ya Maendeleo kwa tija na kuondokana na utegemezi.
Ameyasema hayo katika kikao cha Baraza Maalum la kujadili hoja za Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Seriakali (CAG) kilichofanyika june,13,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Masasi.
Aidha Kanali amesisitiza kuwa endapo Halmashauri zitaweka mfumo mzuri wa kudhibiti vyanzo vyake vya Mapato ya ndani na kurekebisha kasoro zitakazobainika itasaidia kupunguza kasi ya upotevu wa mapato ya serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Masasi Lauter Kanoni amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Serikali ya Wilaya itasimamia kikamilifu fedha zote za Miradi ya Maendeleo zinazotolewa na serikali.
Halmashauri ya Mji Masasi kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 imepata hati Safi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.