Mkuu wa wilaya ya Masasi Claudia Kita ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa michezo mbalimbali na uandishi wa insha iliyoandaliwa na wilaya hiyo katika kuadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika leo Desemba 9 ,2022.
Shamra shamra hizo zimehitimishwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana (Masasi Girls) Jioni ya leo ambapo kwa upande wa mpira wa miguu timu ya MANAWASA imeweza kuibuka washindi wa kwanza Timu ya chuo Cha Maendeeleo (FDC) imeshila Nafasi ya Pili huku timu ya Watumishi ikishika nafasi ya tatu.Kwa upande wa Uandishi wa Insha shule ya msingi Chiungutwa ilifanya vizuri na kwa upande wa shule za sekondari shule ya Masasi kutwa waliibuka washindi huku washindi wa kufukuza kuku,kuvuta kamba na michezo mingine nao walipata zawadi.
Dc Kita amewashuku wananchi na Watumishi wa wailaya hiyo kujitokeza kwa wingi pamoja na kushiriki kwenye shunguli mbalimbali za kijamii kama kufanya usafi,kupanda miti na hata michezo kuanzia Desemba 5 hadi leo Desemba 9 ambapo amewahimiza kuendelea kudumisha amani na utulivu.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.