Katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Mkuu wa wilaya ya Masasi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) mh . Lauter John Kanoni ameweka mipango mikakati ya kuhakikisha na kuwezesha Elimu inapanda kwa kiwango kikubwa.
Mipango mikakati hiyo imewekwa Agost 24,2023 katika kikao cha kamati ya Ushauri ya wilaya kwa kipindi cha januari hadi Juni (DCC).
Mipango hiyo ni pamoja na kujenga Shule maalumu ya sekondari yenye bweni kwa ajili ya wanafunzi ambao watapata alama A watapewa kipaumbele cha kupangiwa kwenye hiyo shule na hiyo ni ni kidato cha kwanza hadi Nne,kutembelea shule zote na kuona changamoto walizonazo ambazo zinazopelekea kufeli kwa wanafunzi na kuanzisha ujenzi wa mabweni kwa shule zote za sekondari za kata.
''kipaumbele changu namba moja ni Elimu na katika hili sitakata tamaa ni lazima Masasi ibadilike kielimu,lazima tubadilike''.
Aidha ameongeza kuwa ili ufaulu uongezeke ni lazima watoto wote wapate chakula Shuleni na wazazi wahamasike kuchangia.
Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya kikao cha ushauri wameahidi kuunga mkono juhudi za mkuu wa wilaya na kuhakikisha elimu bora inapatikana Masasi kwa kushiriki ujenzi wa mabweni ,kuwasimamia watoto kuhakikisha wanaenda shule na kutoa malezi bora kwa watoto.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.