Halmashauri ya Mji Masasi kupitia Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imeendesha zoezi la upuliziaji wa dawa ya kuua mazalia (viluilui) vya Mbu katika maeneo ambayo yanazalisha Mbu ikiwa ni katika kutekeleza kauli mbiu ya “Ziro Malaria inaanza na mimi”.
Hatua hiyo pia, ni utekelezaji wa maagizo ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndg, Godfrey Mnzava aliyoyatoa kwa Halmashauri zote Nchini yaliyolenga kuhakikisha maeneo yote yenye mazalia ya Mbu yanapuliziwa dawa.
Akizungumza wakati wa upuliziaji wa dawa katika eneo la bwawa lililopo soko la machinjio ya kuku, Kata ya Migongo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Afisa Afya Halmashauri ya Mji Masasi, Bw. Christopher Ponela amesema zoezi hilo ni endelevu hususani katika maeneo yote yanayozalisha Mbu.
“Zoezi hili la kupuuliza dawa aina ya Griselesf kutoka TPBL Kibaha ni endelevu, maeneo yanayozalisha Mbu tumeyabaini yote, tumeanza hili zoezi na tutaendelea kwenye maeneo yote tuliyoyabaini ambayo Mbu anaweza akaa, akataga na akazaliana, kimsingi tunashukuru Serikali, Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Mji Masasi na Mganga Mkuu kwa kufanikisha zoezi hili, litaleta tija ya kuondoa kabisa ugonjwa wa Malaria.
Naye, Mkazi wa Migongo, Bi. Yustina Vicent Mathias amesema zoezi hilo limewasaidia sana kupunguza mazalia ya Mbu kwa kiasi kikubwa na hivyo litakwenda kuwasaidia kumaliza kabisa mazalia ya Mbu katika maeneo yao.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.