Agosti 21,2019 Mkurugenzi wa Elimu Msingi Ndg.George Jidanva aliongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja Benki ya Dunia katika ukaguzi wa miradi ya Elimu inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia programu ya EP4R Halmashauri ya Mji Masasi.
Katika ukaguzi huo wajumbe hao wametembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili (2), mabweni mawili (2) pamoja na matundu sita (6) ya vyoo katika shule ya Sekondari Mtapika na shule ya Msingi ya Mfano Kitunda yenye vyumba 17 vya madarasa, nyumba mbili za walimu (1/2), Maktaba, jengo la Utawala, Bwalo la chakula na vyoo matundu 34.
Ujenzi katika shule ya Sekondari Mtapika utagharimu jumla ya TZS 196, 600, 000.00 na Shule ya Msingi ya mfano Kitunda utagharimu TZS 706,400,000.00 hadi kukamilika.
Wakati wakitembelea shule ya Sekondari ya kutwa Mtapika na shule ya Msingi ya mfano Kitunda Mkurugenzi wa Elimu Msingi toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndg.George Jidanva alimshuru Mkurugenzi wa Halmashuauri ya Mji Masasi Bi.Gimbana Ntavyo kwa hatua nzuri ya ujenzi na usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya ujenzi ya shule kama ilivyoelekezwa na serikali.
Naye Mkaguzi wa ndani toka Benki ya Dunia Ndg.Mwakiluma Mkundwa alitoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji Masasi kwa hatua nzuri ya ujenzi waliofika hasa katika shule ya Msingi ya Mfano Kitunda ikiwa ni miongogoni mwa shule nne katika Tanzania zilizopewa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi na kuwa na nyaraka zote za manunnuzi zilizotumika katika manunuzi ya vifaa vya ujenzi.
Pia Afisa Manunuzi toka Benki ya Dunia Ndg.Gisbert alimshukuru Mkurugenzi Bi. Gimbana Ntavyo kwa miradi yote ya shule walizotembela na kusema “Sisi kama wadau wa maendeleo tunashukuru tunapoona mradi unafanyika kama ulivyopangwa”.
Mwisho Mkurugenzi wa Mji Bi.Gimbana Ntavyo aliishukuru Serikali na wafadhili toka Benki ya Dunia kwa kuleta fedha katika ujenzi wa miundo mbinu ya shule hasa ujenzi wa shule ya Msingi ya mfano Kitunda.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.