• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAIS TAMISEMI ANAYESHUGHULIKIA ELIMU NDUGU GERALD G. MWELI, ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA KUWAPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA SHULE YA WASICHANA MASASI

Posted on: May 28th, 2020


Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Masasi Mji

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Ndugu Gerald Geofrey Mweli, ameridhishwa na uwekaji sawa wa miundo mbinu ya Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita wanaotarajiwa kuanza masomo yao siku ya jumatatu ya tarehe 01/06/2020 ikiwa ni agizo lililotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, la kufungua vyuo na Shule za Sekondari kwa wanafunzi wa Kidato cha sita.

Ndugu Mweli, ambaye ametembelea Shuleni hapo leo amewatoa hofu wazazi na walezi kutokana na mikakati thabiti iliyowekwa na Serikali yenye lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira yaliyo salama hasa kipindi hiki ambacho tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa kutokana na janga la ugonjwa wa COVID – 19.

“Wakurugenzi na Wakuu wa Shule, mnapaswa kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wanajengwa kisaikolojia na kuwaondolea hofu ili waweze kuzingatia masomo na akili yao iweze kurudi katika hali ya kawaida” alisema Ndugu Mweli.

Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi Gimbana Emmanuel Ntavyo amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu ya kwamba Halmashauri ya Mji Masasi imechukua tahadhari zote zilizotolewa na Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, na kwamba tayari Halmashauri imeandaa vifaa kinga vya kutosha ili wanafunzi hao waweze kujikinga na ugonjwa wa COVID – 19.

Kabla ya kutembelea Shuleni hapo, Naibu Katibu Mkuu na msafara wake ambao uliongozwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Bi Germana Mung’aho, walitembelea Shule ya Msingi ya mfano Kitunda iliyopo Kata ya Mkuti Halmashauri ya Mji Masasi ambapo Ndugu Mweli alipongeza jitihada zilizofanywa na Halmashauri ya Mji Masasi katika kusimamia ujenzi wa Shule hiyo pamoja na kutoa fedha shilingi milioni sitini na nane (68,000,000/=) kutoka kwenye mapato yake ya ndani ili kuongezea nguvu ujenzi wa shule hiyo. 

Ndugu Mweli, amewataka Walimu wa Shule hiyo ya Msingi Kitunda kufanya kazi kwa bidii ili ubora wa miundo mbinu ya Shule hiyo uendane na ufaulu nzuri kwenye mithani ya Kitaifa.


Ndugu Gerald Geofrey Mweli (Kulia, mwenye koti) akielekea kweye Bwalo la chakula ili kuzungumza na Walimu wa Shule ya Msingi Kitunda




Matangazo

  • MAELEKEZO KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 KWA WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI MASASI September 24, 2019
  • NAFASI ZA KAZI YA KATIBU MUHTASI III NA MTENDAJI WA KIJIJI III June 30, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA UPANGISHWAJI WA MABANDA KWENYE JENGO LA HALMASHAURI YA MJI ENEO LA MKUTI September 18, 2018
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • MKUU WA MKOA WA MTWARA MHESHIMIWA GELASIUS GASPAR BYAKANWA AIPONGEZA HALMASHAURI YA MJI MASASI KWA KUPATA HATI SAFI YA UKAGUZI KWA MWAKA 2018/2019

    June 04, 2020
  • HALMASHAURI YA MJI MASASI KUPITIA IDARA YA AFYA YAENDESHA MAFUNZO KWA WANACHUO WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI MASASI (FDC) JUU YA KUJIKINGA NA COVID-19

    June 01, 2020
  • NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAIS TAMISEMI ANAYESHUGHULIKIA ELIMU NDUGU GERALD G. MWELI, ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA KUWAPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA SHULE YA WASICHANA MASASI

    May 28, 2020
  • Mkuu wa Wilaya ya Masasi akabidhi mabati 20 kwa Shule ya Msingi Mbonde

    May 21, 2020
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.