KITENGO CHA TEHAMA
HALMASHAURI YA MJI MASASI
KITENGO CHA TEHAMA NDANI YA HALMASHAURI YA MJI MASASI KINATEKELEZA
MAJUKUMU YAKE KWA KUFUATA TARATIBU NA KANUNI ZA SERIKALI KAMA
VITENGO VINGINE VILIVYOPO NDANI YA HALMASHAURI YA MJI MASASI
MAJUKUMU YA KITENGO
Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yaliyogawanyika katika sehemu kuu mbili
1. : TEHAMA
Kusimamia Sera, Sheria, Taratibu na miongozo ya Kitengo inayotolewa na
serikali juu ya uendeshaji wa Kitengo cha TEHAMA & Uhusiano
Kuandaa Mpango Mkakati kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
Kuandaa Miongozo na taratibu kwa kuzingatia kwa matumizi salama ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kutengeneza mpango wa matengenezo (Preventive na maintenance plan)
kwa kila mwaka wa fedha na kuutekeleza.
Kuishauri ofisi ya Mkurugenzi juu ya ya masuala yanayohusiana na
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali
mtandao.
Kusimamia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na
utekelezaji wake kwa Halmashauri.
Kutoa na kuratibu msaada wa teknolojia ya habari kwa menejimenti ya
Halmashauri.
Kusimamia na kuratibu kazi za taaluma ya TEHAMA zinazofanywa katika
Vitengo na Idara nyingine.
Kutathimini, kuboresha na kusimamia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye
halmashauri.
Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya
taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa
kujenga uwezo
Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya
teknolojia ya habari na mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na
namna ya kuthibiti.
Kutoa ushauri bora na viwango kwa vifaa vya TEHAMA vinanyo nunuliwa,
kufungwa na vinanyotumika kulingana na viwango vilivyowekwa na
Serikali
Kuandaa na kuisimamia sera ya TEHAMA
Kusimamia Tovuti ya Halmashauri
2. HABARI NA UHUSIANO
1. Kusimamia Sera, Sheria, Taratibu na miongozo inayotolewa na serikali juu
ya uendeshaji wa Mifumo, Miundombinu na vifaa vya Habari na
Mawasiliano katika Halmashauri Kutoa Matangazo yote ya Kazi na Miradi
inayotekelezwa kwenye Halmashauri
2. Kutoa Vijarida, Vipeperushi na Vitambulisho vya kazi kwa watumishi wa
Halmashauri
3. Kutangaza Vivutio vya utalii na Maeneo ya Uwekezaji ya Halmashauri
kwenye Tovuti, Runinga, Magazeti na Redio Kupiga picha za Matukio
mbalimbali yanayotokea katika Halmashauri na Kuyahifadhi kwa ajili ya
Kumbukumbu za Halmashauri
4. Kukusanya na Kuaandaa Habari za Halmashauri
5. Kukusanya habari za Halmashauri zilizochapishwa kwenye Magazeti
mbalimbali
6. Kukusanya na kutunza habari za mtandaoni zinazoihusu Halmashauri kwa
kutumia “Computer” Maalum.
7. Kuboresha mahusiano kati ya Halmashauri, Waandishi wa Habari, Wananchi
na Taasisi nyingine.
ORODHA YA WATUMISHI WA KITENGO CHA TEHAMA
MTAKI MAINDA 0756728613
KAJUTI NYAMBI 0655074924
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.